The House of Favourite Newspapers

Shamsa: Akinipenda Chidi Inatosha!

Shamsa Ford

STAA mwenye mvuto Bongo Muvi, Shamsa Ford amesema kuwa hata kama leo watu watamchukia kwa jinsi alivyo au kwa kuzungumza ukweli hawezi kuumia hata siku moja kwa sababu anaamini aliyempenda kwa dhati ambaye ni mumewe Chidi Mapenzi yupo, inatosha.

 

Staa huyo alizungumza na gazeti hili la Amani baada ya watu wengi kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kutokelezea na nguo fupi kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, na kusema kuwa ni ngumu kumridhisha kila mtu kwenye maamuzi yako.

 

“Mimi Mungu kanijalia maneno sijali kabisa na isitoshe Chidi akinipenda na akakubaliana na maamuzi yangu kwangu inatosha kabisa siwezi kumridhisha kila mtu,” alisema Shamsa.

Vilio,Majonzi! Vyatawala Mazishi ya Mama wa Shigongo

Comments are closed.