The House of Favourite Newspapers

Shamsa amfungukia Nay wa Mitego

FordStaa wa filamu Bongo, Shamsa Ford.

KARIBUNI wasomaji wetu wa kolamu hii ambayo tumekuwa tukiwaletea wasanii mbalimbali na kufunguka mambo ambayo yamekuwa yakikutatiza, kwanza napenda kuomba radhi kwa kutomleta mwanadada, Riyama Ally kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.

Leo hii tunaye staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford ambaye amefunguka mambo mengi ya kisanaa na kimaisha.

nayEmmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’

Msomaji: Habari dada Shamsa kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri lakini ningependa kujua pale unapokumbwa na skendo huwa unajisikiaje au umeshazoea hayo mambo?
Shamsa: Nikiwa kama mzazi huwa najisikia vibaya na bora skendo yenyewe iwe ya kweli ikiwa ya kusingiziwa huwa naumia zaidi.

Msomaji: Eti dada nilisikia unatoka na msanii Emmanuel Elibarik ‘Nay wa Mitengo ‘ mliishia vipi au bado mnaendelea kimyakimya?

Shamsa: Masuala ya Nay tumeshamalizana, kila mtu yupo bize na maisha yake.
Msomaji: Hivi dada maisha yako yapoje baada ya kuachana na baba watoto wako (Dickson) huoni kama mmemuathiri mtoto aliyezoea kupata malezi ya wazazi wote wawili?

Shamsa: Mtoto wangu yupo sawa tu kwa kuwa nampa malezi bora hakuna kilichoharibika.

Msomaji: Wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kuchukizwa na baadhi ya sehemu wanazopangiwa kuigiza, wewe ipi inakupa wakati mgumu?
Shamsa: Kwa upande wangu nafiti kote sina kinachoniwia ugumu.
Msomaji: Unapenda mumeo awe na sifa gani?
Shamsa: (kicheko) awe na hofu ya Mungu, mchapakazi, mwenye upendo na asiwe mtu maarufu.

Msomaji: Ushindani ni mkubwa sokoni bidada, umejipangaje kukabiliana na hilo mwakani?

Shamsa: Nimejipanga ipasavyo kaeni mkao wa kula tu, nakuja na filamu inaitwa Chale Mvuvi na Broken, mtanikubali zaidi.

Comments are closed.