The House of Favourite Newspapers

SHAMSA ATOBOA SIRI YA UBONGE !

Shamsa Ford

STAA wa Bongo Muvi, Shamsa Ford amefunguka kuwa siku zote mwili wake unafumuka pale tu anapokuwa na mawazo tele kichwani mwake, lakini akiwa hana mawazo yoyote kichwani, basi hawezi kunenepa.  Akizungumza na Amani, Shamsa alisema kuwa, tofauti na watu wengine kwamba unaweza kukutana na mtu ukaona amenenepa ukadhani ana furaha, kwa upande wake ni kinyume chake.

“Watu wangu wa karibu kabisa wakiniona nimenenepa wanajua wazi kuwa siko sawa kabisa hivyo hata hawawezi kuniambia shida zao zozote hahaha..,” alisema Shamsa huku akiachia kicheko cha kishkaji.

Comments are closed.