The House of Favourite Newspapers

SHAMSA ATUPA KULE DAYATI!

MWANAMAMA wa Bongo Muvi, Shamsa Ford amesema anajifahamu kuwa yeye ni kibonge, lakini suala la dayati hataki kulisikia.

 

Akistorisha na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Shamsa amesema unamkuta mtu anajinyima kula siku nzima ili akonde, lakini kwa upande wake ni vigumu kufanya hivyo kwa sababu hata akinenepa hakuna kinachoharibika.

 

“Sitaki mtu aniletee habari za dayati hata kidogo kwani sitamuelewa na siwezi kumuelewa kwa sababu ni kujitesa. Mbona mwanamke mnene ni mzuri tu? Hata mimi ninajiona niko poa na ninapendeza sana ninapovaa nguo zangu,” alisema Shamsa ambaye ni mama wa mtoto mmoja.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.