The House of Favourite Newspapers

SHAMSA FORD ‘ASTAAFU’

MSANII wa filamu Bongo, Shamsa Ford amedai kuwa mwaka huu ni mwaka wake wa kustaafu kuvaa nguo za vimini kwani amedhamiria kuwa mwanamke mwenye stara na atahakikisha anawabadili na wanawake wenzake wengine kwa kuwauzia nguo za kiheshima.

 

Akipiga stori na Showbiz, Shamsa alisema anamshukuru Mungu kuuona mwaka huu akiwa mzima na kwa kuwa mwaka mpya unakuwa na mambo mapya, yeye ameamua kubadilika katika suala la mavazi.

 

“Sina sababu tena ya kuendelea kutojistiri kwa sababu Mungu ameniokoa na kunistiri kwa kunipa mume, mwaka huu ni wa kuonesha kuwa mimi ni mama mwenye stara, naamini kwa kuwa na duka la madira na mitandio nitaweza kuwa mwanamke mwenye stara na hii ndiyo njia pekee ya kunipa mwisho mwema hapa duniani,” alisema Shamsa.

 

Shamsa ni staa ambaye maisha yake yote amekuwa akipendelea kuvaa nguo fupi, jambo lililokuwa likimfanya wakati mwingine asemwe vibaya hasa ikichukuliwa kuwa ni mke wa mtu.

 

HAMIDA HASSAN | IJUMAA WIKIENDA

EXCLUSIVE: DJ wa ALIKIBA Afunguka Anavyofanya Nae Kazi!

Comments are closed.