The House of Favourite Newspapers

Shamsa Ford: Siwezi Kurudiana Na Chid Mapenzi

0

MUIGIZAJI kutoka katika kiwanda cha Bongo Muvi, Shamsa Ford amefunguka kuwa hawezi kurudiana na aliyewahi kuwa mume wake ambaye ni mfanyabiashara, Chid Mapenzi kwa kuwa hana tena mapenzi naye.

 

Shamsa amesema alishampa mapenzi yote mumewe huyo wa zamani, lakini alishindwa kuuthamini upendo wake na alivyoamua kuomba talaka maana yake hakuwa tena na mapenzi kwake hivyo itakuwa ngumu kurudi kwake, licha ya kuwa alishamsamehe kwa kila kitu na watabaki kuwa kama kaka na dada.

Hatua hiyo ya Shamsa imekuja mara baada ya Chid Mapenzi kuandika maneno katika mtandao wake wa Instagram ambayo yalionyesha kujutia kumpomteza Shamsa katika maisha yake ambapo alitumia post hiyo kumuomba msamaha mkewe huyo wa zamani.

 

Shamsa aliliambia Championi Jumamosi: “Niliona ile post kiukweli iliniuma sana, kwa sababu inaonyesha ni kiasi gani imemgusa, mimi nilishamsamehe, wala sina tatizo naye kabisa, lakini kurudiana naye tena ni kitu ambacho hakiwezekani na ni jambo ambalo anatakiwa kulifahamu, atabaki kuwa kama kaka na mtu wangu wa karibu.”

STORI NA ISSA LIPONDA, CHAMPIONI

Leave A Reply