The House of Favourite Newspapers

Shamsa: Mastaa Wandeleze Wema wa Mwezi Mtukufu

Shamsa Ford

BAADA ya hivi karibuni wau­mini wa dini ya Kiislamu kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramad­hani, msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford amewataka mastaa kuendeleza yale mema waliyokuwa wakifanya ndani ya mwezi huo na kuachana na kujiachia kihasara.

Akibonga na Za Mo­tomoto News, Shamsa alisema ndani ya mwezi wa Ramadhani watu mbalimbali hasa mastaa walikuwa wakiuhesh­imu kwa kufanya yaliyo mema, kuvaa kiheshima na kutoachia video na picha za ajabu mitandaoni hivyo hata sasa waendelee hivyo hivyo ili kuendelea kumtukuza Mungu zaidi.

“Nawasihi mastaa waendeleze mema waliyokuwa waki­yafanya wakati wa Ramadhani, tusione wakiwa wanakaa nusu utupu au kufan­ya mambo mengine ya ajabu, wafanye ibada sana maana maisha yenyewe ni mafupi mno,” alisema Shamsa.

Comments are closed.