Shamsa: tumalizeni bifu, uchaguzi umeisha

Shamsa_Ford_04.jpgGladness Mallya

STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amewataka wasanii wenzake waliotofautiana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu kumaliza bifu kwani zoezi hilo limemalizika na maisha lazima yaendelee.

Akipiga stori na gazeti hili, Shamsa alisema anamshukuru Mungu yeye hakuwa na bifu na mtu kwa sababu alijua kabisa kuna maisha baada ya uchaguzi ila wenzake waliingia katika migogoro ya kisiasa kwa tofauti za kiitikadi.

“Jamani wasanii wenzangu mliotofautiana na kuwekeana bifu kipindi cha uchaguzi, nawasihi mmalize ili tufanye kazi kwa bidii kwani wakati wote wa kampeni tasnia ya filamu ilikuwa imelala, mimi nimeshaanza kwa kasi ya ajabu na hivi karibuni filamu yangu mpya itakuwa mtaani,” alisema Shamsa.


Loading...

Toa comment