Shamsia Amvaa Waziri Makamba, Atema Cheche – ”Sehemu Inachakatwa Gesi Na Umeme Hakuna”… Video
Mbunge wa Mtwara Vijijini, Shamsia Mtamba (CUF) amesema Waziri wa Nishati, January Makamba ni msikivu kwa sababu alikubali kukaa kikao na wabunge wa Mtwara na kusikiliza kero za wananchi wao kuhusu umeme na kuahidi atashughulikia suala hilo ndani ya siku 90.
Shamsia amesema anamuombea Makamba atimize ahadi yake ili wananchi wa Mtwara waondokane na kero ya umeme kukatikatika.