The House of Favourite Newspapers

Shangwe za Tamasha la Sanaa Kijiji cha Makumbusho Dar leo

siku-ya-msanii-6-001-copyKikundi cha Ngoma za asili kutoka Buguruni Dar kiitwacho Safari Theatre Group kikitoa burudani viwanjani hapo.

siku-ya-msanii-7-001-copyMwanadada akiwarusha vilivyo baadhi ya wananchi ambao wameshafika viwanjani hapo.

siku-ya-msanii-8-001-copyKikundi hicho kikiendelea kutoa burudani.

siku-ya-msanii-9Baadhi ya wananchi waliofika eneo hilo wakifuatilia kikundi hicho cha ngoma.

siku-ya-msanii-1-001-copy-copyWananchi wakiendelea kufuatilia buradani kutoka kwa kikundi hicho.

siku-ya-msanii-3-001-copy-copyMichoro mbalimbali iliomo katika tamasha hilo.

siku-ya-msanii-4-001-copy-copy

Bidhaa mbalimbali zilizomo katika tamasha hilo.

siku-ya-msanii-5-001Miongoni mwa vikundi vitakavyotoa burudani vikiwa katika picha ya pamoja.

HATIMAYE ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani imefika ambapo leo kuanzia asubuhi shangwe za Tamasha la Sanaa Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar zimetawala.

Tamasha hilo, limeonekana kuwa kivutio miongoni mwa wahudhuriaji kutokana na uwepo wa ngoma, Muziki wa Asili, Bongo Flava, Muziki wa Bendi, Matarumbeta, Sarakasi, Vichekesho, Maigizo ya Jukwaani na maonesho ya Sanaa za Ufundi.

Vivutio vingine ambavyo vinavyovutia ni pamoja na  picha za kuchora za mafuta na maji, sanamu za kuchongwa, sanamu za kuungwa kwa vyuma chakavu, vyungu, mikeka, wasusi, ramani na ubunifu wa majengo.

Tamasha hili la sanaa linafanyika kabla ya maadhimisho ya siku ya msanii Oktoba, mwaka huu likiwa na lengo la kuwaweka pamoja wasanii wa fani mbalimbali ili kupata fursa ya kuonyesha kazi zao kwa hadhira, kuweza kujenga uelewa kwa hadhira juu ya kazi zao mbalimbali za sanaa.

Na Denis Mtima/Gpl

 

 

 

Comments are closed.