Sharifa Suleiman Mwenyekiti Mpya Bawacha, Awabwaga Washindani wake
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Sharifa Suleiman ameshinda nafasi ya uenyekiti wa baraza hilo atakaloliongoza kwa miaka mitano ijayo.
Sharifa ameshinda nafasi hiyo baada ya ushindi wa kura 222 katika uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam dhidi ya kura 139 alizopata mshindani wake, Celestine Simba.