SHEHE MKUU AMFUNGUKIA IRENE UWOYA

Sheikh Mkuu wa Mkoa, Alhad Mussa

DAR ES SALAAM: Sheikh Mkuu wa Mkoa, Alhad Mussa amemfungukia Msanii wa Filamu za Kibongo, Irene Uwoya baada ya kutangaza kwamba hakuolewa kwa dini ya Kiislamu na aliyekuwa mume wake, Dogo Janja (AbdulAzizi Chende) ambao wawili hao kwa sasa wamemwagana.  

 

Akiongea na Amani Shehe huyo alisema, kauli ya Uwoya kudai kuwa yeye si Muislamu inaonesha kuwa wakati akibadili hakuifuata dini bali mwanaume.

 

“Mwanadada huyo kuchukua uamuzi wa kutaka kuolewa na aliyekuwa mwenza wake hakuridhia kutoka moyoni, hivyo katika ndoa hiyo Uwoya alimfuata mwanaume na wala hakufuata dini,” alisema shehe huyo.

 

Aliongeza kusema, licha ya kumfuata mwanaume huyo lakini pia mume inawezekana hakumfundisha masuala ya dini kama anavyotakiwa kufanya na ndiyo maana mkewe akaamua kurudi katika dini yake ya awali ambayo ni ya Kikristo.

TUJIKUMBUSHE

Uwoya alifunga ndoa ya Kiislamu na Dogo Janja na kutangaza kuwa, amebadili dini na kuitwa Sheila, hata hivyo baada ya miezi kadhaa wawili hao waliachana kimyakimya bila kuweka wazi ndoa yao kuvunjika.

 

Aidha, baada ya kuwepo kwa uvumi huo, hivi karibuni Uwoya aliibuka na kusema hakuwahi kubadili dini kwa ajili ya kuolewa jambo ambalo shehe amelitolea ufafanuzi.

Toa comment