The House of Favourite Newspapers

Shehe Ponda Awaliza Mashehe, Wanawake

PONDA (5)Shehe Ponda akiongozana na mashehe wengine mara baada ya kuachiliwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro.

Stori: Dustan Shekidele, Morogoro
MACHOZI ya furaha! Sekunde chache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro kumuachia huru Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, mashehe kadhaa na wanawake waumini wa Kiislamu waliofurika eneo hilo, waliangua vilio wakiwa hawaamini kilichotokea mbele yao.

PONDA (3)Mashehe wakionesha nyuso za hudhuni.

Shehe Ponda, aliyekuwa mahabusu kwa kesi ya uchochezi zaidi ya miaka miwili, akituhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, aliachiwa huru Jumatatu ya wiki hii.

Wanawake wa Kiislam wakionesha hudhuni

Mara baada ya Hakimu Mary Moyo kutoa uamuzi huo, kundi la mashehe na wanawake kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro waliangua vilio baada ya kumuona kiongozi wao huyo akitoka katika geti la mahakama hiyo akiwa huru.

PONDA (1)…mama huyu akilia kwa uchungu

“Nafurahi kuwa huru baada ya kuwa nimesota rumande kwa zaidi ya miaka miwili baada ya kukosa haki yangu ya msingi ya dhamana, kwenye kesi hii yenye dhamana ambayo kwa sababu ambazo zisijui, DPP alifunga dhamana yangu, nashukuru kuwa huru na mengi tutazungumza baadaye, ” alisema Shehe Ponda huku akiwa na furaha.
PONDA (4)Baada ya kutoka mahakamni hapo, shehe huyo na kundi la waumini walielekea kwenye Msikiti wa Dini Moja Mungu Mmoja uliopo maeneo ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa kwa ajili ya dua maalum.

Comments are closed.