MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) katika Mkoa wa Kilimanjaro ikishirkikiana na Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Athuman Kihamia, na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo, wamekamata shehena ya simu za mkononi katika mpaka wa Tarakea wilayani Rombo zilizokuwa zikiingizwa nchini bila kufuata taratibu kutokea nchini Kenya.
Simu hizo zimekamatwa baada ya taarifa za kiintelejensia zilizofanikisha gari aina ya Fuso ambalo lilibeba ndizi lakini ndani yake yakawekwa maboksi hayo ya simu zenye thamani ya Tsh milioni 700.
Aidha, watu kadhaa wameshikiliwa na polisi akiwemo dereva wa gari na mama ambaye ndiye aliyekuwa mwenye mzigo wa ndizi akitokea Tarakea kupeleka Dar es Salaam.



