Sheikh Issa Othman Aomba Kujiuzulu Mwenyekiti wa Tume ya Maboresho ya Bakwata
Sheikh Issa Othman Issa, ameandika barua kwa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir ya kujiuzulu katika wadhifa wake wa Mwenyekiti wa Tume ya Maboresho ya Bakwata.
Sheikh Issa aliteuliwa na Mufti Zubeir, Januari mwaka huu kuwa mwenyekiti wa tume hiyo ambayo pamoja na mambo mengine, ilikuwa na jukumu la kuhakiki na kufuatilia mali za Bakwata zilizokuwa zinamilikiwa na watu wengine kinyume na sheria.