Sheikh Kandauma Atoa Onyo Kwa Wanaomdhihaki Snura – Video
MWANADADA Snura Anton Mushi ‘Snura’ aliongea kuhusu kuacha muziki, lakini pia amesema sio muziki tu bali hata filamu hatashiriki na kwa ujumla yeye na sanaa ndio basi tena.
Sheikh Ahmed Kandauma amesema kufuatia uamuzi wa mwanadada Snura Mushi kutangaza kuachana na muziki na kumrudia Mungu, yeyote ambaye ataendelea kupiga au kutazama nyimbo zake, basi atakuwa anapata dhambi.
Akizungumza kupitia Global Radio na Global TV, Sheikh Kandauma amezitaja aya kadhaa zinazoeleza jambo hilo na kuwataka watu kutii kile kilichoombwa na Snura, cha kufuta nyimbo zake na kazi zote za sanaa.