The House of Favourite Newspapers

Sheikh Ponda aachiwa huru

BREAKINGNEWS3

SHEIKHPONDA4

Sheikh Issa Ponda.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya jinai ameachiliwa huru asubuhi hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro.

Akisoma hukumu hiyo ambayo imeahirishwa mara kadhaa, Hakimu Mkazi Marry Moyo amemuachia huru kiongozi huyo aliyekaa rumande kwa zaidi ya miaka miwili baada ya kujiridhisha na vifungu vyote vya sheria.

Baada ya kuachiwa huru, Sheikh Ponda amelakiwa na wafuasi wake waliokuwa wamefurika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro.

Akiongea na wanahabari mara baada ya kuachiwa huru, Sheikh Ponda ameshukuru kwa kuachiwa huru ila akamtupia lawama Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kwa kuzuia haki yake ya msingi ya dhamana na kumfanya akae rumande kwa zaidi ya miaka miwili na kuongeza kuwa mengi atayaongea akipata nafasi.

Baada ya kuongea na wanahabari, Sheikh Ponda ameelekea katika Msikiti wa Dini Moja Mungu Mmoja uliopo eneo la Kiwanja cha Ndege, Morogoro.

Comments are closed.