The House of Favourite Newspapers

Sheikh Ponda Ajisalimisha Polisi Dar

0
Sheikh Issa Ponda.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda mapema leo ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam ‘Central’ akisindikizwa na jopo la wanasheria wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara, Prof. Abdallah Safari na kwenda moja kwa moja kwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa, jana alimpa siku 3 tu Sheikh Ponda, ili kujisalimisha na kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, na iwapo hatafanya hivyo watamchukulia sheria stahiki.
“Ametenda makosa ya jinai kama uchochezi, lakini pia amekuwa anatoa lugha ambazo ni za kejeli, dhidi ya serikali, anatufutwa na kama unamjua mwambie ajisalimishe ili tuweze kumhoji, kukimbia hakutomsaidia, tukiona kuna kosa la jinai tutampeleka mahakamani kama hana tutamwachia, mimi nampa siku tatu lakini akija leo (jana) ni nzuri zaidi, nampa siku 3 ajitokeze mwenyewe aweze kuhojiwa, vinginevyo hatakuwa salama”, alisema Kamanda Mambosasa.
Juzi, Jeshi hilo lilivamia mkutano wa Sheikh Ponda aliokuwa nafanya na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, na kufanikiwa kukamata baadhi ya watu wakiwemo waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo.

Baada ya Kuona Hali ya Tundu Lissu, Sheikh Ponda Azungumza Haya

Leave A Reply