Habari Sherehe ya Maadhimisho ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Day 2022 Ilivyofana Last updated Dec 3, 2022 0 Share Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdor Mpango (kushoto), akipokea tuzo ya shukurani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi Angelina Ngalula, kwa kutambua mchango wa mheshimiwa rais katika mafanikio ya sekta binafsi nchini. Hafla hiyo ilifanyika wakati wa maadhimisho ya siku ya Sekta Binafsi jijini Dar es Salaam . Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki. Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio kwenye sherehe hiyo. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi Angelina Ngalula, akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo. Mmoja wa wadau akipokea tuzo kutoka kwa Makamu wa Rais. Picha ya pamoja mgeni, viongozi mbalimbali na baadhi ya wadau waliotunukiwa tuzo. 0 Share