SHEREHE za Siku ya Wafanyakazi Duniani, leo zimefana jijini Dar es Salaam ambapo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, ameongoza sherehe hizo kwa wafanyakazi mbalimbali walioungana na wafanyakazi kote duniani.
Lyaniva ameongoza maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambapo ameleza kuwa serikali itaendelea kutoa huduma bora na kuwathamini wafanyakazi na kuhakikisha sekta za umma na binafsi zinatatua kero mbalimbali za wafanyakazi.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa sherehe hizo, baadhi ya wafanyakazi wamesema kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na ufanisi lakini wakaiomba serikali ishughulikie kero zao za malimbikizo ya mishahara yao na haki zingine.
Maadhimisho ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu ya “Uunganishaji wa Mifuko ya Jamii Ulenge Kuboresha Mafao ya Mfanyakazi”.
Na Denis Mtima/GPL.
Comments are closed.