The House of Favourite Newspapers

SHEVA AMEPANIA KINOMA MWANANGU

BAADA ya kujihakikishia nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba, mshambuliaji, Miraji Athuman ‘Sheva’ anataka nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Miraji ameibukia kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba, hasa katika kipindi hiki ambacho nahodha wa timu, John Bocco akiwa nje ya uwanja akiuguza majeraha, ambapo katika michezo nane aliyocheza amefunga mabao manne na kutoa pasi tatu.

“Siku zote nimekuwa nikiomba niwe moja ya wachezaji bora wa Tanzania katika kizazi hiki, hivyo kwa nafasi ambayo nimeipata sasa katika klabu yangu na Taifa nitaitumia vizuri ili niendelee kudumu na kuaminiwa zaidi,” alisema Sheva ambaye ni miongoni mwa matunda ya timu ya vijana ya Simba enzi za Seleman Matola.

Comments are closed.