MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Group, Eric Shigongo (kulia) leo asubuhi ameingia barabarani jijini Dar es Salaam akiwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kuuza gazeti jipya la michezo la Sporti Extra.
Shigongo ameuza gazeti hilo akiwa katika eneo la Mwenge ikiwa siku chache tangu lipunguzwe bei kutoka shilingi 800 hadi shilingi 500.
Hii ni wiki ya pili kwa wafanyakazi hao kuingia barabarani katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambapo kwa sasa gazeti hilo bora la michezo litakuwa linatoka mara mbili kwa wiki ambazo ni siku ya Alhamisi na Jumapili kwa bei hiyohiyo poa ya sh. 500.
Katika uuzaji huo Shigongo alilitambulisha gazeti hilo kwa wateja mbalimbali katika eneo la Mwenge ambapo wateja wengi walionekana kuvutiwa nalo kutokana kuwa na stori na makala mbalimbali za uchambuzi wa michezo na burudani.
Shigongo aliwataka wasomaji kuendelea kuliunga mkono gazeti hilo kutokana na kuwa na habari za ndani na nje ya nchi huku akiwaomba wateja hao kuendelea kupeana sapoti Watanzania wenyewe kwa kupenda kununua kazi ambazo zinatengenewa na Watanzania.
“Nadhani ni jambo zuri na hakuna ambaye hanifahamu, leo tupo hapa tunafanya promosheni ya kuuza gazeti letu jipya la michezo la Spoti Xtra, niwaombe tuendelee kupeana sapoti kwa kununua vya kwetu; ndani ya hili gazeti utapata kila kitu kwa bei ya shilingi 500,” alisema Shigongo.
Comments are closed.