Shigongo Amshukuru Juma Aweso kwa kutekeleza miradi maji ya maji ya Buchosa

Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amewashukuru watendaji wa wizara ya Maji inayoongozwa na Juma Aweso kwa kwa kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi maji ya maji ya Bomba na visiwa kwenye Jimbo la Buchosa.
Shigongo Kwa niaba ya wananchi wa Buchosa ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hasani Kwa kuhakikisha unatoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maji.
Wakazi wa Buchosa walikuwa na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama lakini kutoka na Serikali kutoa fedha za kutekeleza miradi ya maji, Kwa sasa wananchi wananeema na wataondokana na tatizo la uhaba wa maji lililokuwa likiwakabili apo awali.
Miradi ya maji ya Bomba ambayo kwa sasa Unatekelezwa kwenye Jimbo la Buchoa ni mradi wa maji wa Bupandwa unahudumia Kata ya Katwe, bangwe na Bupandwa, mradi ya maji wa Kafunzo unahudumia Kata ya Kafunzo, mradi ya maji wa Kazunzu unahudumia Kata ya Kazunzu na Bulyaheke, Mradi wa maji wa Kata ya Bugoro unaohudumia Kata Bugoro na Lugata na mradi wa maji ya Bulyaheke unahudumia Kata ya Bulyaheke.
Visima vinavyochimbwa Buchosa 19 kati hivyo 9 vimekamiika na kufungwa miundombinu maji na vinatumika kati ya hivyo ni pamoja na sukuma na Buswelu.