Shigongo Amshukuru Rais Samia Kwa Mradi Mkubwa wa Maji Maisome
Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo ametiza ahadi ya ujenzi wa mradi mkubwa maji ya bomba utakao huduma wakazi 16983 wa kisiwa cha Maisome kilichopo Jimbo la Buchosa.
Mradi huo nimoja ya ahadi alizozitoa Kwa wananchi wa Maisome juu ya kuwaletea mradi wa maji ya bomba ili kuepuka kushambuliwa na mamba wakati wanapokwenda kuteka maji ziwa Victoria.
” Katika jambo linaloniumiza Mimi Shigongo nikusikia taarifa ya mwananchi kupoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba anapokwenda ziwa Victoria kufanya shughuli za kibinadamu huwa naumia sana ndiyo maana Leo nimeleta mradi maji ili kuondoa adha hiyo kwa wananchi, amesema Shigongo
Kata ya Maisome ni miongoni mwaka Kata 11 kati ya Kata 21 zinazounda Halmashauri ya Buchosa zilizoko kandokando mwa ziwa Victoria ambazo wakazi wake hupoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba wakati wanakwenda kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya ziwa Victoria.
Kisiwa cha Maisome ni miongoni mwa Kata 21 zinazounda Halmashauri Buchosa Ina vijiji vitatu ambavyo ni Kanoni, Busikimbi, Kisiba inaidadi ya watu 16983 na idadi ya kaya 1283
Wananchi wa kisiwa cha Maisome wamempongeza mbunge wa Buchosa Eric Shigongo kwa kuwaletea mradi wa maji ya bomba ambapo utawasadia wakazi hao kuacha kwenda ziwani na kuepuka kuliwa na mamba.
Joyce Amos ni mkazi wa Kijiji cha Kanoni amesema matukio ya watu kupoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba wakiwa ndani ya ziwa Victoria wakioga,Kufua nguo,na kuteka maji yalikuwa yanatokana na ukosefu wa maji majumbani lakini kutokana na mradi huu matukio hayo yatapungua.
Kilio cha wananchi wa Kata Maisome kimeendea kutatuliwa baada ya meneja wa Mamulaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) wilayani Sengerema George Masawe kumutambulisha mkandarasi anatakayetekeleza mradi huo wa maji kwenye kisiwa hicho.
” Mradi huu utetekelezwa ndani ya wiki tatu na chanzo cha maji ni visima virefu ambavyo vitawekewa pampu na matanki kisha mitambo la Sola itasaidia kusukumua na kusambaza kwenye kaya za wakazi wa kisiwa hicho ,amesema Masawe .
Masawe amesema heko za kupatikana Kwa fedha za mradi huu zimemwende mbunge wa Buchosa Eric Shigongo aliyepigana kupata fedha na hatimaye mradi inatekelezwa .