The House of Favourite Newspapers

Shigongo Apandikiza Mbegu ya Ushindi kwa Madereva Bajaj – Video

MKURUGEZNI Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo,  amepandikiza mbegu ya ushindi kwa madereva wa Bajaj wa kituo cha Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kupata fursa ya kuzungumza nao mapema leo Jumatatu, Oktoba 1, 2018.

Akizungumza na madereva hao, Shigongo amewaeleza kuwa hata wao wana nafasi na uwezo mkubwa wa kutoboa kimaisha, kwani miaka ishirini iliyopita hata yeye alikuwa akiuza karanga mitaani na maisha yake yalikuwa kama wao.

Ili wafanikiwe kama yeye, Shigongo amewasihi madereva hao kuweka akiba, kuanzisha miradi mingine midogomidogo ili kuwa na vyanzo vingi vya mapato na kubana matumizi yao na hata kipato kinapoongezeka matumizi yao YABAKI VILE VILE kama walivyokuwa na kipato kidogo.

Amesisitiza kuwa hakuna sababu ya wao kujikatia tamaa ya kwamba labda wanafanya biashara hiyo kwa vile hawana elimu ya kutosha.  La hasha! Aliwaambia, elimu siyo chanzo cha mafanikio bali  ni maarifa tu na hivyo wasikatee tamaa.

 

Akijitolea mfano mwenyewe, Shigongo amewaeleza kwamba sababu ya yeye kuwa na magazeti yasiyopungua msnane ambayo ni Championi, Spoti Xtra, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Risasi Mchanganyiko, Uwazi, Amani,  ni kwamba alifanya hivyo ili kutengeneza vyanzo vingi vya mapato na hivyo waendelee kumuunga mkono kwa kununua magazeti hayo.

Kwa upande wao, mmoja wa waendesha Bajaj eneo hilo la Mwenge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Bajaj, Sudi Madunda,  amempongeza Shigongo kwa namna alivyofika eneo hilo na kuwatia moyo pasipo kuonyesha hali yake ya kipato kama matajiri wengine, ambapo yeye anatumia elimu na mbinu za kibiashara kuwaelimisha wao na watu wengine namna ya kutengeneza pesa na hivyo wakamtaka aendelee kufanya hivyo kila mara atakapopita eneo hilo.

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Shigongo Apandikiza Mbegu ya Ushindi kwa Madereva Bajaj

Comments are closed.