The House of Favourite Newspapers

Shigongo Apania Kujenga Buchosa Mpya, Amwaga Mamilioni – Video

0

 

MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo ametembelea miradi ya maendeleo katika Kata ya Bulyeheke na kuongea na wananchi wa kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Mbugani.

 

Akiwa Bulyeheke ambayo ina jumla ya vijiji vinane na vitongoji 34, Shigongo amesema katika kipindi kifupi cha uongozi wake (takribani siku 120) tayari kata hiyo imepokea jumla ya shilingi miliioni 227 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Fedha hizo pamoja na nguvu za wananchi zinatumika kwenye ujenzi wa zahanati, vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari, matundu ya vyoo, ofisi za walimu, wodi ya mama na mtoto ambapo miradi hiyo imeashaanza kutekelezwa katika vijiji na vitongoji vyote vya Kata ya Bulyeheke.

 

Amesisitiza kwamba katika kipindi kifupi tangu achaguliwe amefanya mambo mengi kutokana na ushirikiano anaopata kutoka kwa wananchi wa jimbo hilo, hivyo amewaomba kuendelea kujitolea kuiunga mkono serikali ili kujiletea maendeleo kwani haiwezi kufanya kila kitu peke yake bali kwa kushirikiana na wananchi.

 

“Nimekuta hapa mmejenga shule yenu mpya, mmesomba mawe, matofali mmeacha kazi zenu kwa sababu mna uchungu na elimu za Watoto wenu, mmekamilisha madarasa nane, mimi nimeweka zaidi ya shilingi milioni 11 kuenzeka madarasa hayo na kuyamalizia ili Watoto wetu waanze kwenda shule.

 

 

“Sozswa tumeweka Tsh milioni 50, na ndani ya siku 120 za Rais Magufuli, tayari Buchosa tumepata Tsh milioni 257 kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali. Lengo la Serikali ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake, hivyo sisi kama wananchi tunapaswa kuisapoti Serikali kwa kujitolea ili tuendelee kujiletea maendeleo,” amesema Shigongo.

 

Leave A Reply