The House of Favourite Newspapers

Shigongo awatia moyo wanafunzi

0

Shigongo akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani)

Shigongo akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani).

Shigongo akiwa na baadhi ya wanafunzi

Shigongo akiwa na baadhi ya wanafunzi.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, S.G Lugano akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani)

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, S.G Lugano akizungumza na wanafunzi (hawapo pichani).

Baadhi ya wanafunzi waliokusanyika mahali hapo wakimsikiliza Shigongo.

Baadhi ya wanafunzi waliokusanyika mahali hapo wakimsikiliza Shigongo.

Wanafunzi wanaounda SYB wakiwa na shingo katika picha ya pamoja

Wanafunzi wanaounda SYB wakiwa na shingo katika picha ya pamoja

Stori: Mwandishi Wetu
Mhamasishaji maarufu nchini Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo amewatia moyo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa iliyopo jijini Dar es Salaam katika semina iliyofanyia shuleni hapo Jumatatu iliyopita kwa kuwapa mbinu mbalimbali za kufaulu na kuwa viongozi wakubwa hapo baadaye.
Akizungumza hayo mbele ya wanafunzi zaidi ya mia tano shuleni hapo, Shigongo alisema kwamba ili kufanikiwa na kuwa mtu fulani, mwanafunzi anatakiwa kupambana, kuzingatia muda na kuacha mambo yote ambayo si ya msingi katika elimu yake.
“Unapoamua kupambana, hautakiwi kufanya vitu ambavyo si vya msingi, kama una rafiki ambaye unahisi anakurudisha nyuma badala ya kusonga mbele, muepuke, kama unafanya kitu ambacho hakikupeleki mbele zaidi ya kukurudisha nyuma achana nacho,” alisema Shigongo.
Semina hiyo fupi ambayo iliandaliwa na kikundi cha wanafunzi cha S.Y.B (Scan Your Brain) ilihudhuriwa pia na mwalimu mkuu wa shule hiyo, S.G Lugano ambaye naye aliwapa wanafunzi hao mbinu mbalimbali za kufanikiwa katika masomo yao.

Leave A Reply