The House of Favourite Newspapers

Shigongo: Nampenda Diamond, Aendelee Kuwekeza ‘Usiku Unakuja’ – Video

MKURUGENZI Mtendaji wa makampuni ya Global Group, Eric Shigongo,  amesema msanii Diamond Platinumz hatakuwa kinara wa Bongo Fleva milele hivyo zama zake zitapita na watakuja wasanii wengine watakaoanzia alipoishia na kuendeleza tasnia hiyo.

 

Shigongo aliyasema hayo jana Jumapili wakati wa hafla iliyoandaliwa na kampuni ya Global Publishers kuwashukuru wasomaji wa magazeti yake, wauzaji (mavenda) na mawakala wa magazeti hayo.  Hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar es Salaam.

 

Kauli hiyo ya Shigongo ilikuja baada ya kuulizwa swali wakati akifanya mahojiano na Global TV Online iwapo alishawahi kumsaidia jambo lolote Diamond kwani staa huyo amemtaja Shigongo kama mmoja wa ‘role model’ (mtu aliyempa hamasa ya mafanikio) wake.

“Sikumbuki kama nilishawahi kumsaidia, watu wananiambia lakini mimi sina kumbukumbu, labda kuandikwa magazetini kwa ajili ya promosheni za kazi zake za muziki, pengine kutokana na nasaha zangu ambazo huwa nazitoa kuwashauri Watanzania wenzangu na kuwapa mbinu za kujikwamua kwenye umaskini,” alisema Shingongo na kuongeza:

 

“Ninachoweza kumwambia tu ni kwamba apambane.  Unajua ukifanikiwa unapata marafiki wengi, na wengi wao wanakuwa wanataka pesa zako au cheo chako, siku pesa zikiisha hutowaona tena. Ametoka kwenye umaskini, asisahau alikotoka.

 

“Walikuwepo akina Mohamed Ali, wakaondoka, wakaja kina Tyson, wakaondoka, sasa hivi yupo Maywether, ataondoka atakuja mwingine. Mimi nipo, nitaondoka.   Je, nikiondoka watoto wangu wataendelea kula chakula kilekile? Watasoma shule zilezile? Lakini pia tulikuwa nao akina Mr. Nice, waliondoka, sasa hivi yupo Diamond, itafika wakati ataondoka, watakuja wengine, hatakuwa championi milele.

 

“Ninachoweza kumwambia ni kwamba awekeze kwa ajili ya baadaye, ukiwapelekea watu chakula sehemu uliyotoka, Tandale,  watasema unatafuta kiki, ukila peke yako Madale watasema huyu jamaa mbinafsi, mimi namshauri asisikilize watu wanasema nini, aendelee kupambana hadi mwisho,” alisema Shigongo.

 

VIDEO: SHIGONGO AKIMZUNGUMZIA DIAMOND

Comments are closed.