The House of Favourite Newspapers

‘Shilingi milioni tatu zinaniua

0

Stori: Nyemo Chilongani

Bado hali ya msichana aitwaye Ted Mallya (23) imeendelea kuwa mbaya kutokana na kukosa msaada wa kutosha kutokana na kusumbuliwa na kidonda kilichokuwa katika mguu wake wa kulia.

Akizungumza na mwandishi wetu katika ofisi za gazeti hili zilizopo Bamaga, Mwenge, jijini Dar es Salaam, Ted amesema kwamba amekuwa akizunguka huku na kule kutafuta msaada lakini kote huko hakupata fedha ambazo zimekuwa zikihitajika katika matibabu yake.

SIKIA KILIO CHAKE
“Nilikuja kwa mara ya kwanza hapa katika ofisi zenu (Global Publishers), mkanitoa kwenye gazeti lakini kiasi nilichokipata, hakikuweza kunisaidia. Ninawaomba sana Watanzania wanisaidie kwani ninateseka kwa maumivu makali.

“Nasumbuliwa na kidonda kilichopo mguuni na tatizo hili lilianza mwaka 2007 kwa kuvimba mguu ambapo mishipa ya damu inayoshusha damu chini haipandisha damu juu, kitu kilichoufanya mguu kuvimba.”

Baada ya kuona tatizo hilo, Ted anasema aliamua kwenda hospitali mbalimbali hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo madaktari walimtahadharisha kwamba hakutakiwa kusababisha kidonda chochote katika mguu huo lakini kwa bahati mbaya, alichomwa na mti kitu kilichomsababishia kidonda hicho.

“Baada ya kupata kidonda moyo wangu ulihuzunika sana na sasa napata maumivu makali na nashindwa kulala. “Ninateseka, mguu unauma mno, kila siku ni lazima nitoke niende kutafuta msaada mitaani, huko, wapo wanaonisaidia na wengine hawana.

Kiasi ninachokihitaji ni shilingi milioni tatu ili nisafirishwe kwenda India nikatibiwe. Naamini nikikosa hizo shilingi milioni tatu, nitakufa, fedha hizo zitaniua,” anasema Ted huku akibubujikwa na machozi.

Kwa yeyote anayeguswa na tatizo la Ted, anaweza kumsaidia kupitia namba 0754 395 622 au akaunti ya benki, CRDB namba 0152317004200. KUTOA NI MOYO.

Leave A Reply