Shilole adaiwa kupangiwa jumba na kigogo!

HAMIDA HASSAN NA IMELDA MTEMA

UBUYU! Taarifa iliyotua kwenye Dawati la Ijumaa Wikienda inadai kuwa, mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amepangiwa bonge la jumba maeneo ya Kijitonyama, Dar, huku kigogo mmoja Bongo (jina kapuni) akitajwa kujitwisha jukumu hilo.

Hata hivyo, Shilole ambaye ni mpenzi wa Nuh Mziwanda amecharukia madai hayo na kusema kuwa, ni kweli amehamia kwenye nyumba hiyo iliyopo Kijitonyama lakini pesa yake ndiyo imetumika na si mchepuko kama watu wanavyodai.

“Mh! Watu hawaishi kunisema na kunitungia maneno, mimi nafanya kazi na huu mjengo nimepanga kwa pesa zangu, huyo pedeshee anaanzaje kuwa na mimi wakati nina mtu wangu jamani?” alihoji Shilole.


Loading...

Toa comment