The House of Favourite Newspapers

Shilole Atamba kwa Shoo za Nje

Shilole na Nuh Mziwanda wakiwa jukwaani

Na BONIPHACE NGUMIJE| GAZETI LA UWAZI| SHOWBIZ

MWANADADA asiyekauka kwenye media ambaye ni Mwanamuziki na Muigizaji Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa yeye ndiye msanii wa kike Bongo anayeongoza kwa shoo za nje.

Akipiga stori na safu hii ya burudani Shilole alisema kuwa ndani ya miezi miwili hupiga shoo zaidi ya mbili wakati mwingine hufi kisha hadi nne jambo ambalo halifanywi na msanii yeyote wa kike.

Zuwena Mohammed ‘Shilole

“Jaribu kufuatilia ni msanii gani kwa sasa Bongo anapiga shoo nje kama mimi, jibu ni kwamba hayupo, mimi ndiye napiga shoo zaidi za nje, mwezi ujao natarajia kupiga shoo Swaziland na bado nina mipango mingi tu ya kukamua nje,” alisema Shilole.

Alipoulizwa kuhusu mkwanja anaovuta kwenye shoo hizo na  jinsi anavyopata mashavu hayo ya shoo, hakuweka wazi akidai atawafungua wapinzani wake.

Comments are closed.