The House of Favourite Newspapers

SHILOLE AWAPA SOMO MASTAA WALIOMUIGA

Zuwena Mohamed ‘Shilole’

KUTOKANA na wimbi la mastaa wa kike kuzidi kujiingiza kwenye upikaji wa vyakula ‘mama lishe’, staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kuwatahadharisha kwa kuwa yeye ndiye aliyeanza kabla ya wote.  

 

Akibonga na Amani, Shilole alisema anafurahi kuona kile alichoanzisha kinaigwa na wasanii wenzake wengi ila tahadhari ni kwamba wanatakiwa kukomaa sana kwani vitu vya kuiga bila kuwa na misingi imara watashindwa.

 

“Ni sawa wameniiga wengi lakini wanatakiwa kuwa na misingi imara vinginevyo wataanguka, nimekuwa mfano wa kuigwa kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuanzisha mama lishe kwa kufungua mgahawa ndiyo wengine wakafuata hivyo watambue kuwa aliyeanza kaanza tu, niko kwenye biashara hii kwa miaka mitatu sasa hivyo naamini hakuna wa kunishinda,” alisema Shilole.

 

Mastaa ambao wameanzisha biashara hiyo baada ya Shilole ni wengi akiwemo, Esha Buheti, Sabrina Rupia ‘Cathy’

Stori: Gladness Mallya

Comments are closed.