Shilole Ayapa Kisogo Mapenzi!

Msanii na mmiliki wa Shishi Food anayefanya poa kwenye miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, kwa sasa ameyapa kisogo mapenzi na badala yake, yuko bize na kazi ili heshima yake isitetereke.

 

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Shilole au Shishi Baby ambaye siku chache nyuma alimwagana na aliyekuwa mumewe; Ashraf Uchebe, amesema kuwa, ameona akiyaweka tena mapenzi mbele, hayatamzalishia matunda yoyote mazuri, lakini akikazana katika kazi yake, inamletea mafanikio makubwa kuliko mapenzi.

 

“Jamani kwa usawa huu mtu usipobadilika na kuangalia kitu cha maana cha kufanya, ni shida sana.

“Mimi mambo ya mapenzi sasa hivi yanisubirie kwanza nifanye kazi zangu ili nipate maendeleo na siyo mapenzi ambayo kila kukicha wanafaidi mashabiki wa Instagram kukuangalia maisha yako,” anasema Shilole ambaye kesi yake na Uchebe inaendelea mahakamani.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Toa comment