Shilole: Bado Nahangaikia Kiingereza, Kitaeleweka tu

MWANAMUZIKI na mjasiriamali, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameeleza kuwa, hajisikii aibu anapopewa maiki na kuzungumza Kingerezabroken’ kwa sababu anajua huko mbele hakuna msanii atakayemfikia kwa lugha hiyo.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shilole alisema ipo siku atashika maiki watu watashangaa atakapozungumza Kingereza kilichonyooka na ndio maana kila kukicha anakazana bila kuchoka.

 

“Nitazungumza broken mpaka kieleweke wala sitakaa nikaona aibu kwani ni lugha ya kimataifa na naamini itanikutanisha na watu mbalimbali,” alisema Shilole ambaye siku hizi amekuwa akiongea Kiingereza broken anapokuwa mbele za watu.

Stori: Imelda Mtema.


Loading...

Toa comment