The House of Favourite Newspapers

Shilole, Barnaba Usiku wa Wabishi… Kuimba Wapo na Nay Dar Live

0

NA MWANDISHI WETU | RISASI JUMAMOSI | MIKITO NUSUNUSU

KWA mara ya kwanza tangu Ngoma ya Wapo iliyofanywa na mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ itoke, inatarajiwa kuimbwa kwa pamoja na wakali wa muziki huo, Barnaba na Shilole Jumamosi ijayo, Mei 20 ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Shilole

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Nay aliyewahi kuwika pia na ngoma kibao kama Shika Adabu Yako na
Muziki Gani alisema, usiku huo unaotambulika kama Usiku wa Wabishi, wakali kibao watatoa burudani ya nguvu kwa mtonyo mdogo wa 5,000 tu getini.

Barnaba

“Ni shoo ya kuleta amani na upendo. Shoo ya kufurahia na wanangu wote wa Ilala, Temeke, Kinondoni na Kigamboni. Siyo shoo ya kitoto kwani mbali na kuimba Ngoma ya Wapo kwa pamoja, kutakuwa na sapraizi kibao,” alisema Nay na kuongezea kuwa burudani hiyo itatawaliwa na staa wa vichekesho, Mkali Wenu.

Nay Wa Mitego – WAPO (Official Music Video)

Leave A Reply