Shilole kumchora Nuh kalioni

shilole (1)
STAA
wa mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema ana mpango wa kuchora tena jina la mpenzi wake, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kwenye moja ya kalio lake ikiwa ni njia mojawapo ya kuonyesha mapenzi yake ya dhati kwake.

shilole (2)Akizungumza na mwandishi wetu, Shilole alisema kuwa Nuh amemchora jina lake kwa ukubwa sana na yeye kuonyesha jinsi gani anamthamini, ameona si vibaya kama atamchora ‘tatoo’ nyingine kwenye kalio tofauti na ile ya awali ambayo amemchora kifuani.

“Mimi bado tatoo moja ya muhimu sana ambayo nataka kuchora kwenye kalio ili kuonyesha ni jinsi gani nampenda mpenzi wangu Nuh,” alisema Shilole.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Loading...

Toa comment