Shilole: Nina Ujauzito

USIKU wa jana katika hafla ya mama-kijacho, Aunty Ezekiel, muigizaji wa filamu na mjasirimali Shilole amefunguka kuwa na yeye ni mama-kijacho mtarajiwa. Alisema maneno hayo alipokuwa akiongea na wageni waalikwa katika shughuli hiyo

Hivi karibuni muigizaji huyo amekuwa akidaiwa kuwa na mahusiano na mpiga picha aitwaye Rommy. Hata hivyo, wawili hao hawajawahi kukiri kuwa ni kweli au la.

 

Awali Shilole alikuwa mke wa kijana Uchebe ambaye kwa sasa ni kama mtu na adui yake kwa kile kinachodaiwa Shilole alikuwa akipokea kipigo cha mara kwa mara kutoka kwa mumewe. Hata hivyo, baadhi ya wadau wamesema huenda mimba ikawa ni ya Uchebe.

Toa comment