Shilole: Rostam Wakileta Mimi Naweka

WAKILETA naweka! Ndivyo aliyosema staa wa Muziki wa Mduara, Shilole ikiwa imepita wiki chache tangu itoke Ngoma ya Kijiwe Nongwa ya wakali Roma Mkatoliki na Stamina (Rostam) ambayo ndani yake wame-muimba.

 

Katika ngoma hiyo ambayo ni gumzo kwa sasa kila kona, Shilole ame-maindi kuimbwa tofauti pamoja na mumewe, Uchebe huku akiwaambia ni bora wangemshirikisha mapema.

 

“Malipo ni hapahapa, mbona wasanii wapo wengi kwa nini hawajawaimba? Mbona wameniimba mimi na mume wangu sana. Sasa wakati huu wameshajua kwamba dada hajapenda na ndiyo maana nimewapa sapraiz (ngoma yake mpya ya Sitaki Mazoea) tena nasikia wanamtafuta hadi kesho aliyeniandikia. Nawaambia tu wakileta mimi naweka, wao si wameanza, mimi namaliza,” alisema Shilole.


Loading...

Toa comment