The House of Favourite Newspapers

SHILOLE: SIJAINGIA KWENYE NDOA KUCHEZA MDUARA!

MWANAMUZIKI wa mduara Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, watu wasimfikirie ameamua kuingia kwenye ndoa kama maonesho, bali amedhamiria kwenda kuwa mke anayestahili kuwa mfano wa kuigwa na hatarajii kutoka kwenye ndoa ng’oo. Akizungumza na Amani, Shilole alisema anajua wazi watu wengi wanamuhesabia siku kama ilivyo kwa mastaa wengine, lakini atawashangaza walimwengu wenye kusubiri ndoa za watu kuvunjika.

“Najua wazi watu watakuwa wananihesabia siku ndani ya ndoa yangu, lakini ukweli ni kwamba nitawashangaza watu wengi sana na sina sababu ya kuacha kuwa mke bora na mwenye heshima kwa mume wangu watanihesabia hadi watachoka wenyewe maana mimi nakomaa,” alisema Shilole.

Comments are closed.