The House of Favourite Newspapers

Shilole: Siwezi Kuolewa na Mume wa Mtu

0
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

MSANII wa Miondoko ya Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa watu wajaribu kuziba midomo yao kutokana na ishu yake ya kudaiwa kutaka kuolewa na mwanaume wa mtu aitwaye Uchebe na kusema kuwa angekuwa wa mtu asingeenda kwake.

Akizungumza na Star Mix, Shilole alisema kuwa anashangazwa na watu ambapo wakiona mtu yuko na mtu f’lan ndipo wanaibuka na madai tele kitu ambacho hakiwezi kumsumbua hata siku moja.

“Waseme wanavyoweza wala siwezi kutetemeka kwa hilo na sidhani kama naweza kuolewa na mume wa mtu na kama angekuwa mume wa mtu asingekuja kwangu,” alisema Shilole.

 

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Full Video: Ndege Iliyowabeba Watoto wa Lucky Vincent Ikitua Kutoka Marekani

Leave A Reply