Shilole ‘Siyo Mwenzetu Tena’, Alamba Shavu Kupitia Mama Lishe
Shilole ‘Siyo mwenzetu tena, baada ya kutangazwa na Kampuni ya Gesi ya Oryx imemtangaza Mama Lishe Zuwena Mohamed maarufu Shilole (Shishifood) kuwa balozi wao katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kupikia kupitia mitungi ya gesi nchini jambo lilisemwa na watu wa mjini kuwa hapo sasa amelamba shavu zito kupitia kazi yake hiyo ya Mama Lishe.
Oryx imefikia kumpa staa huyo wa filamu na Bongo Fleva Ubalozi ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu ambaye ameweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania iwe inatuminia nishati safi ya kupikia.
Akizungumza kwenye tukio hilo lililofanyika Julai 4 kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo na Masoko wa Oryx Gas Shaban Fundi amesema wameamua kumchagua Shilole kwasababu ni miongoni mwa wadau wanaohamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Amesema kupitia kwa Shilole wanaamini kuna wengine ambao walikuwa nyuma kwenye matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kuendelea kutumia gesi za Oryx kupikia.
“Tunafamu Shilole amekuwa mjasiriamali maarufu machi, anamiliki migahawa ya Shishifood katika miji ya Dar es Salaam na Dodoma, amekuwa mama Lishe wa kisasa na muumini mzuri wa kutunza mazingira,hivyo Oryx tunaona fahari kumtangaza Shilole kuwa balozi wetu katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kwa pamoja kufikia malengo ya Rais Samia ya kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.”
Kwa upande wake Shilole ambaye pia ni Msanii maarufu nchini,amesema yupo tayari kushirikiana na wadau wengine kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Amesema Kampuni ya Oryx imekuwa ikiweka jitihada kubwa kuhamasisha matumizi nihati safi ya kupikia kwa Mama lishe na baba lishe nchini, hivyo ameona kuna umuhimu mkubwa wa kutoa ushirikiano.