Shilole Tumbo lalazua minong’ono

 12105212_1686065048295221_224609236_nMwigizaji Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

Stori: Musa Mateja
KITUMBO cha mwigizaji Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kimezua minong’ono ya aina yake kutoka kwa mashabiki na mastaa mbalimbali na kuwafanya wengi wao wabaki wakibishana kuwa mrembo huyo atakuwa katundikwa ujauzito na mchumba wake Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.

10004223_1661488030757168_1462718299_nTukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwa Nasibu Abdul ‘Diamond’, aliyekuwa akisherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa ndipo wambeya walipoanza kumsengenya Shilole chinichini.
“Huyu atakuwa kanasa si bure,” alisikika mmbeya mmoja ambaye hakujitambulisha.
Alipoulizwa Shilole kama ni kweli amenasa ‘kibendi’, alijibu:
“Jamani sina mimba, watu watambue tu kwamba hiyo picha nilikuwa nimetoka kula, lakini pia wajue kwamba siku nikipata mimba watajua tu maana nitapiga picha za kutosha,” alisema Shilole.

Loading...

Toa comment