The House of Favourite Newspapers

SHILOLE WANAOFICHA WATOTO WATAUMBUKA WOTE

Image result for Zuwena Mohamed ‘Shilole’
Zuwena Mohamed ‘Shilole’

BAADA ya sakata la mwanamama Rose Alphonce ‘Muna Love’ la kukana kwamba hana mtoto mwingine zaidi ya marehemu Patrick Peter kisha akaumbuka baada ya mtoto kuanikwa, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameeleza kuwa mastaa wa kike wanaoficha watoto wataumbuka wote.

Akichonga na Za Motomoto News, Shilole alisema hakuna siri duniani na wasanii wa kike ambao wamekuwa wakiwaficha watoto wao na kusema hawajawahi kuzaa au walizaa wakafa, ipo siku wataumbuka, pia wanatakiwa kutambua kuwa wanakosa riziki kwa sababu ya kuwaficha malaika hao wa Mungu.Image result for MUNALOVE

“Hakuna siri duniani, ipo siku Mungu atawaumbua wote wanaodanganya kwamba hawana watoto au wamekufa, kuficha malaika hao wanakosa riziki ambazo wangepata kupitia wao, jamani wanawake wenzangu badilikeni, kuwa na mtoto au watoto siyo kashfa ni baraka maana wapo wanaotafuta wanakosa,” alisema Shilole.

Comments are closed.