The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Bado Inazidi Kupeta Mitaa Mbalimbali

0
Msomaji akikabidhi kuponi ya Shinda Nyumba baada ya kuijaza.

KWA uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Amani, inaonesha kuwa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili bado inazidi kupeta siku hadi siku kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar na hata mikoani.

Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda ambaye ndiye mratibu wa promosheni ya Shinda Nyumba, amesema kuwa bahati nasibu hiyo bado ni gumzo kubwa kwa wananchi wa kada zote ambao ni wasomaji wakubwa wa magazeti ya kampuni hiyo.

“Ni wazi kuwa wasomaji wa magazeti yetu ya Ijumaa, Risasi, Amani, Uwazi, Championi na Ijumaa Wikienda wanaifuatilia kwa umakini bahati nasibu hiyo, kila wakala ninayewasiliana naye mikoani anazungumza kuhusu nini kinaendelea, kwa maana hiyo natumia fursa hii kuwafahamisha wasomaji wetu kuwa mambo yanaendelea kuwekwa sawa.

Mr Shinda (katikati) nyumba akiwa katika picha ya pamoja na wasomaji.

“Tumeanza kuboresha zawadi zetu kwa kadiri tunavyokwenda, katika droo zetu tatu ndogo ambazo tumeshazifanya, jumla ya pikipiki tatu zimeshatolewa, televisheni kubwa flat screen tatu pia, dinner set tatu na simu za smartphones nyingi tu. “Tunawasihi waendelee kusoma magazeti yetu ambayo licha ya bahati nasibu hiyo, pia yanawaletea habari motomoto za kijamii, michezo, burudani na za mastaa mbalimbali.

Wasomaji wakichangamkia magazeti ya Global Publishers ili wajaze kuponi za shinda nyumba na kujaribu bahati yao.

“Kwenye magazeti yetu yote, katika kurasa za pili zipo kuponi zenye maelekezo ya namna ya kufanya, ukishamaliza kujaza, unaweza kuzituma kwetu kupitia kwa mawakala wetu waliopo nchi nzima na wale wa Dar es Salaam wanaweza kuja ofi sini kwetu, Bamaga Mwenge na kuziacha kwenye ndoo maalum ya kukusanyia kuponi,” alisema Mkanda.

Naye Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema kampuni inaendelea kuboresha zawadi kwa washindi wa droo ndogo kwa kadiri inavyowezekana ili kuhakikisha watu wanabadili maisha yao kupitia bahati nasibu hiyo ambayo hivi sasa ni gumzo.

“Tupo katika uboreshaji wa zawadi hizi wakati tukiendelea na droo ndogo zitakazofuata, kwa hiyo wasomaji waendelee kusoma magazeti yetu na kukata kuponi kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu hiyo na huenda wakafanikiwa kubadili maisha yao,” alisema.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.

Leave A Reply