The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Droo Ndogo…Mshindi wa pikipiki kupatikana leo

0

3.Rehema Said (kulia) mkazi wa maeneo ya Mbande akishiriki kujaza kuponi ili kuingia katika droo ya Shinda Nyumba. 12. Mmoja wa akina mama lishe akionekana kushiriki kuweka kuponi yake ya Shinda Nyumba. SHINDA NYUMBA (10)NA MWANDISHI WETU, Risasi Mchanganyiko

HATIMAYE ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wasomaji wa Magazeti Pendwa na Championi ya kufanyika kwa droo ndogo ya mwisho ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba imewadia, ambapo leo katika Viwanja vya Manzese, Bakhresa kutachezeshwa droo na mshindi wa kwanza ataibuka na pikipiki aina ya Skymark.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Afisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda alisema kuwa droo hiyo ambayo itakuwa ya nne tangu kuanza kwa droo ndogo itakuwa droo ndogo ya mwisho kabla ya kufanyika kwa droo kubwa ambapo mshindi atajinyakulia nyumba yenye samani zake iliyopo Salasala jijini Dar.

“Tunaendelea kuwashukuru wote wanaoshiriki na washindi wote ambao wamepatikana tangu kuanza kwa droo hizi.

Katika droo ya tatu iliyopita mshindi wa kwanza Zalika Ally kutoka Lushoto, Tanga alijipatia TV flat screen na king’amuzi chake na leo tunatarajia kupata mshindi wa pikipiki,” alisema Mkanda.

Katika droo ya leo, mbali na mshindi wa kwanza kukabidhiwa pikipiki, mshindi wa pili atajipatia simu ya kisasa ‘smartphone’, wa tatu, seti ya vyombo vya jikoni, wa nne mashuka na mwisho tutatoa ving’amuzi vitano kwa washindi watano,” alisema Mkanda na kuongeza kuwa droo kubwa inatarajiwa kuchezeshwa mwezi ujao.

Leave A Reply