The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba ilivyochangamkiwa Mabibo Dar

0

9

Muuzaji wa magazeti (kushoto) akimsaidia msomaji (katikati) kujaza kuponi yake baada ya kununua gazeti la Championi.

8

Mshiriki wa Bahati nasibu ya Shinda Nyumba akiweka kuponi yake.

7.

Vijana wanaofanya shughuli za kusafirisha bidhaa za vyakula kutoka mikoani katika soko la Mabibo wakimtazama mwenzao jinsi alivyokuwa akijaza kuponi yake.

6

Zoezi likiendelea la kujaza kuponi katika soko la Mabibo.

5

Baadhi ya wasomaji wa Magazeti ya Championi Jumamosi na Risasi Jumamosi wakisaidiwa kujaza kuponi zao mara baada ya kununua magazeti kwa muuzaji wa Kampuni ya Global (katikati).

4.

Mama lishe, Husna Bakar wa soko la Mabibo (katikati) akijaza kuponi yake kushiriki droo ya Shinda Nyumba. Anayemwelekeza kulia ni Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.

3

Daima Khalifa anayefanya biashara zake katika soko la Mabibo (kushoto) akijaza kuponi yake ili kushiriki droo ya Bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

2.

Fadhiri Issa anayefanya shughuli zake katika soko la Mabibo (anayejaza kuponi) akishiriki zoezi la Bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

1

Juma Waziri (kulia) mmoja wa wakazi wa Dar aliyekuwa katika soko la Mabibo akielekezwa na Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (katikati) namna ya kujaza kuponi yake.

Daima Khalifa anayefanya biashara zake katika soko la Mabibo (kushoto) akijaza kuponi yake ili kushiriki droo ya Bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

WAKATI Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd ikiendelea kushika kasi, wakazi wa soko la Mabibo jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita walionekana kuvutiwa nayo baada ya kujitokeza kwa wingi kuchangamkia magazeti ya kampuni hiyo kwa kununua magazeti na kujaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu hiyo.

Mara baada ya maofisa wa Global Publishers kufika soko la Mabibo, wafanyabiashara na wanunuzi wakiwemo wabeba mizigo walijitokeza na kununua magazeti ya Global kisha kujaza huku pia walijipatia zawadi za kofia zenye nembo ya Shinda Nyumba zilizokuwa zikitolewa.

Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema: “Wanachotakiwa kufanya wafanyabiashara wa soko hilo ni kununua magazeti ya Global na kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya magazeti hayo ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi Jumamosi na Ijumaa ambayo huuzwa kwa shilingi mia tano na msomaji anaweza kujishindia nyumba ya kisasa, kila anayejaza kuponi nyingi anajiongezea nafasi ya kujishindia nyumba na zawadi nyingine,” alisema Mkanda.
Naye Ofisa Masoko wa Kampuni ya Shinyanga Emporium, Herman Bernad ambao ni wadhamini wa Bahati Nasibu hiyo na ni wauzaji wa pikipiki aina ya Sky Mark na Bajaj za Piaggio, alisema kuwa pikipiki bado zipo nyingi licha ya mwezi uliopita kupatikana mshindi mmoja.
Mshindi huyo, Lucy Swai wa Kibaha alijishindia pikipiki aina ya SkyMark baada ya kushinda katika droo ndogo ya pili na Bernad akasisitiza; “Pikipiki hizo ni bora zaidi kwa matumizi ya familia na hata kwa shughuli za kufanyia biashara kama bodaboda.”alisema.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply