The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Kibamba Hapatoshi Leo

0

Na Mwandishi Wetu | IJUMAA WIKIENDA

WAKAZI wa mitaa ya Kibamba na vitongoji vyake, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, leo watakuwa wenyeji wa promosheni ya Bahati Nasibu kubwa ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, wakati kruu zima likiongozwa na Mr Shinda Nyumba litakapovamia na kufanya shoo.

Shoo hiyo itafanyika maeneo mbalimbali jijini Dar yakiwemo Temeke Veternary, Mwembeyanga, Mbagala, Kizuiani, Manzese, Kigogo, Mburahati, Mabibo, Kimara, Ubungo na Tabata.

“Leo hii tutakuwa maeneo ya Kibamba, tutapita katika mitaa na vitongoji vyote kuanzia Mbezi Mwisho, tukiwa katika promosheni hiyo, tutatoa zawadi nyingi kwa wasomaji ambao tutawakuta na magazeti yetu mawili yanayotoka leo ambayo ni Championi Jumatatu na Ijumaa Wikienda,” alisema mmoja wa maofisa wa kruu hiyo ya promosheni, Keffa Masaga na kuendelea;

“Tutakuwa tumeongozana na Mr Shinda Nyumba katika shoo hiyo ambayo itakuwa ni wakati muafaka kwa wasomaji wa magazeti ya Global Publishers kujitokeza na kuona kitu gani tumekwenda nacho. Ni nafasi pekee kwa wasomaji wetu wa mitaa hiyo kuja kumuona kijana mwenye urefu wa aina yake.”

Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda ambaye ndiye mratibu wa promosheni ya Shinda Nyumba, ameliambia Ijumaa Wikienda kuwa bahati nasibu hiyo bado ni gumzo kwa watu mbalimbali ambao ni wasomaji wakubwa wa magazeti ya kampuni hiyo.

“Kama wanavyojua tumeanza kuboresha zawadi zetu kadiri tunavyokwenda, katika droo zetu tatu ndogo ambazo tumeshazifanya, jumla ya pikipiki tatu zimeshatolewa, televisheni kubwa flat screen tatu pia, dinner set tatu na simu za kisasa nyingi tu.

 

“Tunawasihi waendelee kusoma magazeti yetu ambayo licha ya bahati nasibu hiyo, pia yanawaletea habari motomoto za kijamii, michezo, burudani na mastaa mbalimbali.

“Kwenye magazeti yetu yote, katika kurasa za pili zipo kuponi zenye maelekezo ya namna ya kufanya, ukishamaliza kujaza, wanaweza kuzituma kwetu kupitia kwa mawakala wetu waliopo nchi nzima na wale wa Dar es Salaam wanaweza kuja ofisini kwetu, Bamaga Mwenge na kuziacha kwenye ndoo ya kukusanyia kuponi,” alisema Mkanda.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.

Leave A Reply