The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Yatikisa Chalinze

0
Ofisa Usambajazi wa Global Publishers, Jimmy Haroub akimuelekeza msomaji jinsi ya kujaza kuponi ya Shinda Nyumba.

 

BAHATI Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili leo imetikisa ilipotembelea eneo la Chalinze mkoani Pwani ambako wasomaji wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi wameyachangamkia magazeti hayo kwa wingi.

Msomaji akisoma magazeti ya Championi na Ijumaa.

 

Akizungumza na globalpublishers.co.tz, Meneja Masoko wa Global Publishers, Alex Mabula, amesema lengo la msafara huo lilikuwa ni kuwahamasisha wasomaji wa maeneo hayo kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba ili waweze kuibuka washindi kwenye droo kubwa ya ambapo mshindi ataibuka na nyumba mpya na fenicha zake ndani.

 

Meneja Masoko wa Global Publishers, Alex Mabula, Jimmy Haroub akimuelekeza msomaji jinsi ya kujaza kuponi ya Shinda Nyumba.

 

“Kama tungeweza, tungefika kila eneo kuwahamasisha wasomaji wa magazeti yetu waendelee kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kwa kununua magazeti yetu, kukata kuponi na kututumia. Hapa tulipo tunaelekea mwishoni kabisa mwa tukio hili ambalo zawadi kubwa ya nyumba inaenda kutolewa.

 

Jimmy akimuelekeza msomaji jinsi ya kujaza kuponi msomaji.

 

“Tukiwa Chalinze, tumekutana na wasomaji wa Kibaha, Ruvu hadi Mlandizi, wasomaji wetu wameyachangamkia kwa sana magazeti yetu ya leo Ijumaa ambayo ni Gazeti la Ijumaa na Championi Ijumaa, ambapo wamejaza kuponi zilizopo ukurasa wa pili wa kila gazeti,” alisema Alex.

Msomaji akijaza kuponi.

 

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya washindi wa droo ndogo ya tano kukabidhiwa zawadi zao katika tukio lililofanyika kwenye ofisi za Global Publishers zilizoko Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Wasomaji wakijaza kuponi za Shinda Nyumba.

 Miongoni mwa washindi waliopatikana katika droo hiyo ndogo ya tano ni Geofrey Shangalawe wa Kigoma aliyejishindia seti moja ya televisheni kubwa ‘flat screen.’

Mr shinda Nyumba akiwasaidia wasokmaji kukata kuponi.

NA ISSA MNALY | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply