The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba yawa kivutio Goba, Dar

0

1.Mwanahamisi Kasimu (kulia) mkazi wa maeneo ya Goba Dar akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shionda Nyumba.Anayeshuhudia ni Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda.

Mwanahamisi Kasimu (kulia), mkazi wa maeneo ya Goba Dar akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.

3.Yohana Mkanda (katikati) akijaribu kuwapa maelekezo ya jinsi namana msomaji wa magazeti ya Global anavyoweza kujishindia nyumba.

Yohana Mkanda (katikati) akiwapa maelekezo ya jinsi ya kujaza kuponi wasomaji wa magazeti ya Global ili waweze kujishindia nyumba na zawadi nyingine.

4.Mkanda (katikati) akitoa maelekezo kwa wasomaji wa Gazeti la Uwazi kabla ya kujaza kuponi zao na kushiriki,kushoto ni Abdallah Ally Kibendela na kulia ni Nalimi Bundala.

Mkanda (katikati) akitoa maelekezo kwa wasomaji wa Gazeti la Uwazi kabla ya kujaza kuponi zao na kushiriki, kushoto ni Abdallah Ally Kibendela na kulia ni Nalimi Bundala.

5.Mmoja wa washiriki wa Droo ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba mkazi wa eneo la Goba mwisho akiweka kuponi yake.

Mmoja wa washiriki wa Droo ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba mkazi wa eneo la Goba Mwisho akiweka kuponi yake.

8.Mmoja wa waendesha Bodaboda eneo la stendi ya daladala ya Goba Dar akijaza kuponi yake huku Ofisa Masoko wa Globa akifuatilia zoezi hilo.

Mmoja wa waendesha bodaboda eneo la stendi ya daladala ya Goba Dar akijaza kuponi yake huku Ofisa Masoko wa Globa akifuatilia zoezi hilo.

9.John Andrew (kulia) mkazi wa maeneo ya Goba Dar akijaza kuponi yake ili kushiriki droo hiyo.

John Andrew (kulia) akijaza kuponi yake ili kushiriki shindano hilo.

10

Zoezi likiendelea la kujaza kuponi.

11.

Mkanda (katikati) akimuelekeza msomaji namna ya kujaza kuponi.

12.

Wasomaji wakiendelea kuweka kuponi zao ili kushiriki habari nasibu hiyo.

6.Kevin Aloyce Mkazi wa eneo la stendi ya daladala ya Goba akijaza kuponi yake ili kushiriki droo ya Shinda Nyumba.

Kevin Aloyce Mkazi wa eneo la stendi ya daladala ya Goba akijaza kuponi yake ili kushiriki droo ya Shinda Nyumba.

7.Wakazi wa maeneo ya Goba jijini Dar wakihamasikia kujaza kuponi zao na kushiriki droo ya shinda nyumba.

Wakazi wa maeneo ya Goba jijini Dar wakihamasika kujaza kuponi zao na kushiriki droo hiyo.

2.Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda (katikati)akikagua kuponi kama zimejazwa ipasavyo na wasomaji wa Gazeti la Uwazi, Joyce Mghase (kushoto) na Theodora David.Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda (katikati) akikagua kuponi kama zimejazwa ipasavyo kutoka kwa wasomaji wa Gazeti la Uwazi, Joyce Mghase (kushoto) na Theodora David.

WAKATI Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba ikizidi kushika kasi, wakazi wa Goba jijini Dar leo wameonekana kuvutiwa nayo baada ya kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa kujishindia nyumba hiyo kwa kununua magazeti na kujaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu hiyo.

Mara baada ya maofisa wa Global Publishers kufika Goba, wananchi wengi walijitokeza na kununua magazeti ya Global kisha kujaza uku pia walijipatia zawadi za kofia zilizokuwa zikitolewa.

Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema: “Mnachotakiwa kufanya wakazi wa Goba ni kununua magazeti yetu ya Global na kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya magazeti hayo ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi Jumamosi na Ijumaa ambayo huuzwa kwa shilingi mia tano na msomaji anaweza kujishindia nyumba ya kisasa, ukijaza kuponi nyingi unajiongezea nafasi ya kujishindia nyumba na zawadi nyingine,” alisema Mkanda.

Naye Ofisa Masoko wa Kampuni ya Shinyanga Emporium, Herman Bernad ambao ni wadhamini wa Bahati Nasibu hiyo na ni wauzaji wa pikipiki aina ya Sky Mark na Bajaj za Piaggio, alisema kuwa pikipiki bado zipo nyingi licha ya wiki iliyopita kupatikana mshindi mmoja.

Mshindi huyo Lucy Swai wa Kibaha alijishindia pikipiki aina ya SkyMark baada ya kushinda katika droo ndogo na Bernad akasisitiza; “Pikipiki hizi ni bora zaidi kwa matumizi ya familia na hata kwa shughuli za kufanyia biashara kama bodaboda.”

(Picha/Habari: Denis Mtima/Gpl)

Leave A Reply