The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Yawapagawisha Mashabiki Juve, Madrid

0
Mr Shinda Nyumba akigawa magazeti ya Global kwa watazamaji wa mechi ya Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Italia.

Na Mwandishi Wetu| Uwazi | Shinda Nyumba Awamu ya Pili

TIMU nzima ya Promosheni ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili ambayo ilikamilisha droo ndogo ya nne Jumatano iliyopita katika Viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki ilivamia mpambano wa kukata na shoka baina ya miamba miwili ya Ulaya, Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Italia.

Miamba hao walikuwa wakicheza mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Wales huko Cardiff, Wales, mchezo ambao ulionyeshwa katika televisheni, huku wadhamini wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, Kampuni ya Ving’amuzi ya Ting, ikionyesha bure katika maeneo ya Tegeta Nyuki jijini Dar.

Mr Shinda Nyumba akiwa katika picha ya pamoja na wasomaji wa magazeti ya Global huko Tegeta.

Katika mchezo huo ambao Real waliibuka kidedea, Ting waliwakusanya mashabiki wa soka wa timu hizo katika uwanja huo wa Nyuki, Tegeta ambapo licha ya kufaidi pambano hilo bure, lakini pia walipata fursa ya kujua kuhusu ving’amuzi vyao ambavyo vinafanya vizuri katika soko hivi sasa.

Wakati Ting wakifanya hivyo, mashabiki pia walipata fursa ya kujipatia bure Magazeti ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, ambalo lilikuwa na habari nyingi kuhusu mpambano huo wa kukata na shoka.

Aidha, baadhi ya mashabiki waliojitokeza kiwanjani hapo walipagawa baada ya kumuona Mr Shinda Nyumba akigawa magazeti hayo na baadhi yao kuomba kupiga naye picha.

Jumatano iliyopita, wakati wa uchezeshaji wa droo ndogo ya nne ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, ving’amuzi vitano vilitolewa kwa wasomaji wa magazeti ya Global Publishers.

Washindi hao watano ni Doctor Lihemba (Dodoma), Verus Kweyamba (Moshi), Ally Ramadhan Kazi (Mburahati, Dar), Rhoda Kimenyi (Moro) na Rhoda Mbuya (Uyole Mbeya) ambao watapewa zawadi zao katika muda wa siku chache zijazo utakaotangazwa na uongozi wa Global Publishers, ambao ni wazalishaji wa magazeti ya Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi, Uwazi, Risasi na Amani.

Katika droo hiyo ndogo iliyokuwa na mashamsham mengi kutoka kwa wasomaji waliojazana uwanjani hapo, Peter Katua wa Ilala Dar alijipatia zawadi ya dinner set huku Ally Halifa Kachenje akijipatia zawadi ya simu ya kisasa aina ya Phantom 6, na Shaaban Ngao wa Tabata jijini Dar es Salaam alijidai na pikipiki.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Tecno Mobile, King’amuzi cha Ting, British School na Kilimanjaro Institute of Technology.

Leave A Reply